Description
Mwandishi mmoja mashuhuri hapa duniani aliwahi kuandika katika kitabu chake, ëNo Money Smellsí, kwamba hakuna pesa zinazonuka. Lakini mwandishi wa riwaya hii anadai ìzipo, na zanukaî. Ni pesa zipi hizi? Na vipi zinuke? Hii ni riwaya nzito ya kihistoria. Mwandishi anaivulia jamii miwani na kuitazama kwa makini bila uoga, huku akimulika unafiki na ukatili uliofichika katika mioyo ya wengi. Hata anakutana na huyu ambaye anaambiwa: ìUmemuua mwanao … Lazima umle … î Ni riwaya ambayo itakutoa machozi!





Reviews
There are no reviews yet.